Kiswahili Swahili

Jump to each language

Je, unahitaji msaada wa tatizo la kisheria?

Msaada wa Kisheria Queensland (Legal Aid Queensland) unaweza kukusaidia kwa matatizo mengi ya kibinafsi ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kama unashtakiwa kwa kosa la jinai, mipango ya uzazi ikiwa unatengana, unyanyasaji wa nyumbani na familia, ulinzi wa mtoto, kupinga ubaguzi na madeni.

Masaa: Saa 2.30asubuhi -10.30jioni (8:30am—4:30pm) Jumatatu hadi Ijumaa

Huduma zetu za kisheria bila malipo ni pamoja na:

  • huduma ya siri ya taarifa za kisheria
  • kikao cha ushauri kutoka kwa wanasheria waliohitimu
  • machapisho ya bure kuhusu matatizo ya kisheria.

Msaada wa kisheria na uwakilishi unaoendelea mahakamani inaweza pia kupatikana ikiwa unastahiki.

Unaweza kufikia huduma zetu za kisheria bila malipo kwa kupiga simu 1300 65 11 88.

Interpreter icon

Pata usaidizi katika lugha yako

Ikiwa unahitaji mtu anayezungumza lugha yako mwenyewe, piga simu kwa Huduma ya Utafsiri na Ukalimani kwa nambari 13 14 50 na uombe mkalimani. Waulize kupigia Legal Aid Queensland kwa 1800 998 980. Hii ni huduma ya siri na isiyolipishwa.

Msaada kwa watu wenye matatizo ya kusikia au kusema

Iwapo wewe ni kiziwi au una matatizo ya kusikia au kusema, unaweza kuwasiliana nasi kwa kutumia Huduma ya Kitaifa ya Usambazaji Relay (National Relay Service). Ili kupiga simu, nenda kwenye tovuti ya National Relay Service na kuomba 1800 998 980. Hii ni huduma ya siri na isiyolipishwa.

Last updated 14 July 2023